GET /api/v0.1/hansard/entries/1276886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1276886,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276886/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Zamzam Mohammed (",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kubwa, mgao wetu ni mdogo sana na Wabunge wana mgao wao alhamdulillah mzuri sana. Lakini sisi tumepewa kaunti kubwa kuzunguka na pesa kidogo wakati pesa zingine zinaingia kiholela katika dockets ambazo hatuoni zafanya kazi gani. Ikiwa wanaweza kuelekeza mapeni katika docket moja ile waulize mama Zamzam, kama mama kaunti tuliweka pesa za sodo, hebu tupatie hesabu tuangalie umepeleka skuli ngapi, zimebaki ngapi na ziliisha vipi? Lakini, tunavyozungumza watoto kule Mwakirunge wanatumia matawi ya mnazi kujihifadhi katika mambo ya hedhi. Kwa sababu gani? Skuli za kule hazijafikiwa na sodo. Mamilioni yalitangazwa hapa katika Bunge hili yametoka ili kuweza kununua sodo. Sisi tunaomba, hata zikija katika docket yetu ya gender, waangalie vizuri ziwe zitafikia akina mama wa kaunti arobaini na saba kwa sababu tunaelewa haya maswala. Mambo ni mengi lakini mimi husema ukweli na nitarudia kusema ukweli siku zote. Wapwani tunahangaika na mambo ya title deeds zetu ambazo zinaibiwa humu Nairobi. Mabwenyenye wanaangalia ni shamba gani kule Mombasa ambalo halina title deed . Mzee wa miaka mia moja amekaa katika shamba lake na anafurushwa. Anaambiwa kuna mtu amechukua lile shamba na yeye ndiye ana title deed . Sisi tumesema mara nyingi, hii serikali iangalie wakaazi wa Pwani ndiyo waweze kupewa hati miliki na kujiona kama Wakenya. Isiwe kuwa Pwani si Kenya. Hatutaki kuimba wimbo huo. Tunataka tuseme Pwani ni Kenya tukipata hati miliki. Asante sana Mhe. Spika wa Muda."
}