GET /api/v0.1/hansard/entries/1277039/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1277039,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1277039/?format=api",
"text_counter": 345,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": "Kuna mambo ya utofauti wa makabila ambayo inaitwa ethnicity and diversity kwa lugha ya kimombo. Mimi nimetoka katika Kaunti ya Kwale ambapo kuna vijana wengi ambao wamesoma vizuri sana. Lakini, kupata nafasi katika wizara za kitaifa ni kazi ngumu sana. Wengi wao hawana watu wa kuwashika mkono. Serikali zilizopita… Pia, tuna wasiwasi kuwa Serikali iliyopo itapatia kipaumbele watu kutoka makabila makubwa. Ningeomba Kenya iwe na uwiano na itambue makabila madogo ambayo hayajawahi kuingia katika daftari za uongozi na ajira za kitaifa. Tuna jambo linatendeka katika Kaunti ya Kwale. Tuna uwanja mdogo wa ndege ulioratibiwa kuwa uwanja mkubwa. Suala linalotia utata ni kuwa hawajapeana ardhi kwa upanuzi wa uwanja wa ndege mdogo wa Ukunda ambao upo katika eneo la watalii wengi. Wangekuwa wanatua pale. Mashamba ya watu wa sehemu ya Mkwakwani, Ukunda, yalifanyiwa utafiti 1974 ikaonekana wale wananchi wana haki ya kulipwa ule wanja kwa sababu ni wao. Kulifanywa utafiti mwingine mwaka wa 1984. Kukaja tafiti nyingi mwaka wa 1984 na miaka kumi baadaye, hao watu wakaambiwa mashamba yale si yao. Kuna mzungu anayeitwa Mackenzie ndiye mwenye shamba. Mhe. Spika wa Muda, dhuluma hizi za kijinsia na kibinadamu ambazo zimetendeka haswa katika Kaunti ya Kwale zitakwisha lini? Ninamshukuru mwenyekiti wa kamati ambayo imeleta Ripoti hii na kuangazia pakubwa dhuluma ambazo zinatendeka. Wakwale wamedhulumwa pakubwa na mambo ya mashamba. Wamenyan’ganywa mashamba yao. Ukienda ufuo wa bahari kutoka sehemu inayoitwa Mwembeni mpaka kule Kinondo, utapata mashamba yote yanamilikiwa na watu wa Nairobi. Hawa watu hawajawahi kukanyaga mashamba yale lakini wanayamiliki. Hizi dhuluma zitakwisha lini? Ni wakati mwafaka wa Serikali iliyopo, ikiwa inajigamba inafanya kazi, kuwasaidia wananchi wa taifa hili. Iangalie sehemu ya Kwale ambayo imedhulumiwa pakubwa sana. Hususan, mambo yanayotia uchungu ni mashamba na ajira. Ninaishukuru hii kamati kwa kuileta Ripoti hii. Nimeongea kwa haraka kwa sababu ya kuchunga wakati. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ninaunga Ripoti hii mkono."
}