GET /api/v0.1/hansard/entries/1277350/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1277350,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1277350/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la ziada. Waziri wa Masuala ya Ndani na Utawala wa Taifa, tunayo imani na wewe. Tunayo imani utaleta mabadiliko. Umesema usajili wa wanajeshi uko huru, lakini kuna Wakenya ambao wanakatazwa kujiunga na jeshi kwa sababu ya kimo chao na siyo eti ni wagonjwa. Wanavaa viatu na suruali, na wana afya njema lakini wanakataliwa kwa sababu ni wafupi. Ni Mungu amewaumba hivyo. Kwa nini mnawanyima fursa ya kujiunga na jeshi? Kama mnawaona ni wafupi, wanaweza kumfikia adui bila kuonekana."
}