GET /api/v0.1/hansard/entries/1277423/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1277423,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1277423/?format=api",
"text_counter": 368,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana. Kwanza, pongezi Mhe. Waziri. Siku ya leo umefanya sura zetu kuwa na furaha kwa sababu unajibu kwa ufasaha. Mhe. Waziri, tumeona clip ikizunguka kwenye mtandao wa yule Brigadier, ama sijui ni nani, wa Sudan akiwapa vitisho. Ningependa kujua kama tuna uhusiano mzuri ama ilikuwa na maana gani? Pia, ningetaka kujua jambo kuhusu watoto wetu waliopotezwa Mombasa wakishukiwa kuwa ni Al Shabaab ilhali hawakupelekwa kortini wala hawajapatika hadi leo. Unafanya mbinu gani ili wazazi wao wajue kama wamechukuliwa hatua ama wako wapi hawa wapendwa wao? Asante sana Mhe. Waziri."
}