GET /api/v0.1/hansard/entries/1277910/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1277910,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1277910/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "na hazina nyingine. Nimesikiliza wenzangu wakizungumzia sababu ambazo pesa hizo zinapotea. Mmoja wa wanenaji alisema kuwa hazina hizi zote ziwekwe mahali pamoja. Ikiwa Mheshimiwa anasema kuwa pesa zinapotea katika Uwezo Fund, YouthEnterprise Development Fund, Equalisation Fund na nyingine, tukimwekea yule mwizi anayeiba pesa hizi zote kwa pamoja, si tutakuwa tumemrahisishia kazi ya kuiba? Kama Mbunge wa Jomvu, ningependekeza kuwa hazina hizo zibaki vile vile, lakini pesa ziongezwe zaidi. Kama alivyosema Mhe. C.J., yule aliyeanzisha mambo haya alikuwa na nia njema. Usimamizi ndio unaofanya mambo ambayo hayaeleweki. Kwa hivyo, pesa hizo zibaki katika Uwezo Fund, Youth Enterprise Development Fund, Marginalisation Fund, na"
}