GET /api/v0.1/hansard/entries/1277916/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1277916,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1277916/?format=api",
"text_counter": 281,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "pili. Kwa hivyo, usishangae. Ni kweli kuwa wengine watakapokuja, utatoa mfano kwao kuwa kile Mhe. Kaluma amesema ni kweli. Pesa za Uwezo Fund huwa zinatengwa. Lakini ukitafuta ile miradi ambayo vikundi vilivyopewa pesa vilifanya, huwezi kuiona. Ndiyo maana mwaka 2017, wakati polls zilikuwa zimenikata kidogo, niliita timu yangu ya kampeni na kuwauliza haja yetu ya kufanya kampeni ilhali kulikuwa na vikundi vingi tulivyovipatia pesa wakati huo. Tulikuwa tumewapatia wengi pesa na wakajikimu. Lakini kwa sababu ya usimamizi mbaya, wanaosimamia bodi hawatuletei maafisa wa kutosha wa kuzunguka ili kuona ni vikundi gani ambavyo vimepata pesa za kufanya maendeleo. Isitoshe, jambo hilo ndilo linasababisha vikundi hivyo visiweze kulipa pesa ili vikundi vingine vipate pesa za Uwezo Fund . Mpaka leo, ukiuliza katika eneo bunge lako kama kuna matatizo ya Uwezo Fund na Youth Enterprise Development Fund, unambiwa ati file inatafutwa. Ulimwenguni watu wako dijitali lakini wao wanachakura faili zilizojaa vumbi. Kwa hivyo, ni lazima mambo kama haya yaangaliwe. Ndiyo maana Ripoti hii imeletwa na dada yetu Mhe. Fatuma ambaye hakulala usiku na mchana ili kuhakikisha tumerekebisha mambo haya."
}