GET /api/v0.1/hansard/entries/1277917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1277917,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1277917/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Kuna ukweli na ninataka niseme ambao si siasa. Hazina ya Pesa kwa Vijana inalenga vijana wetu ambao hawajiwezi. Kabla vijana hawa kupewa pesa, huwa wanachunguzwa kwanza kuteua ni wanaweza kupewa pesa zile. Vikundi vya vijana ambao hawajiwezi ndivyo vinapewa pesa hizi ili vijana waweze kujiendeleza na wapate kujikimu kimaisha. Lakini kuna Hustler Fund ambayo ukiwa nyumbani, tajiri ama maskini, una uwezo wa kutumia kidole chako kupata pesa hizo. Ningependa kushauri kuwe na pesa za kumlenga mtu ambaye hajiwezi na za kumlenga anayejiweza. Tunataka pesa hasa zilenge wale ambao hawajiwezi, kwa maana wale ambao wanajiweza wana pesa zao. Mimi ni Mbunge kwa awamu yangu ya tatu. Kabla kuwa Mbuge, nilikuwa Diwani kutoka 2007 mpaka 2013. Kwa hivyo, niko na miaka 16 katika uongozi. Kwa nini nisimwachie mtu mwengine mambo ya pesa za vijana? Pesa za Hustler Fund zinasaidia watu ambao sio walengwa. Wale ambao ni walengwa waweze kusaidiwa kupitia pesa hizi."
}