GET /api/v0.1/hansard/entries/1277918/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1277918,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1277918/?format=api",
"text_counter": 283,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Katika Eneo Bunge la Jomvu, watu wanaotaka kupewa pesa mwanzo hufanyiwa uchunguzi. Wakifaulu, kabla wapewe pesa wanapewa mafunzo. Hakuna maafisa wa kutekeleza mafunzo. Mhe. Catherine na kikundi chake wanasema ni vyema kwa sababu ninasema ukweli. Katika Eneo Bunge langu la Jomvu, tumeshirikiana na Equity Bank inayoongozwa na ndugu yangu Bw. Kanyi ambaye mkurugenzi wake ni James Mwangi. Wanatufanyia mafunzo kuhusu usimamizi wa fedha. Lakini kazi hii ilikuwa ifanywe na maafisa hawa ambao wanagawa pesa hizi. Hii ndiyo maana unagundua vikundi vinajikusanya tu, pengine hata ni afisa fulani akute watu wake kumi kumbe ni majirani zake na wengine ni wapenzi wake, kisha anawashikanisha na kutoa mistari ya kutongoza kupitia kwa pesa za Hazina ya Vijana. Mambo haya ni lazima tutoboe kwa sababu siyo sawasawa. Rusha mistari yako lakiniā¦"
}