GET /api/v0.1/hansard/entries/1278114/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1278114,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278114/?format=api",
    "text_counter": 134,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia kwa hii Hoja muhimu. Kuna aya katika Quran, na haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu kwa sisi Waislamu kwa kitabu chetu kitukufu Quran, inayosema kullu nafsin dai katul maut . Sote tutaionja mauti. Kwa hivyo, hili si suala la mjadala na sote tunajua hasa kwa sisi Waislamu kwamba mtu anapokufa, mambo manne lazima yafanyike. Haya ni kumwosha, kumvika sanda, kumsalia na hatimaye kumzika. Hili tulifahamu vizuri, kumzika sio kumchoma kama vile wengine wanaozungumza. Kwa sisi ambao tuna imani dhabiti ya dini na hii nina imani ni sote Waislamu na Wakristo, tunajua ukifa hima utaenda peponi ama utaenda motoni. Sasa hata ikawa moja ana imani kwamba yeye ni mtu wa motoni, sioni haja kwamba aanze kuchomwa akiwa hapa. Hili pia ni jambo lingine ambalo linashangaza. Pengine mwenyewe unajua kwamba moja kwa moja utaenda motoni lakini unatuambia tuanze kukuchoma hapa hata kabla siku ya hukumu. Hili ni jambo la kushangaza na halipo katika imani ya dini zote ambazo zinatumika. Pengine wenzetu Wahindi ama wale wanaotaka kuchomwa labda tayari hao hawaamini kwamba kuna njia nyingine isipokuwa tu kubaki motoni. Lakini kwa Mkristo na Muislamu, hili ni jambo ambalo haliingii akilini. Kwa hivyo, kuzika ni lazima."
}