GET /api/v0.1/hansard/entries/1278115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278115,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278115/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Nina imani kwamba wakati Langata ilipoanzishwa, haikuanzishwa kwa watu wa Langata. Ilianzishwa wakati huo ikiwa Nairobi na Nairobi ilikuwa na watu wachache mwaka wa 1958. Na ninaimani ilipowekwa pale iliwekwa ikiwa mbali na mji, haikuwa katikati ya mji kama vile ilivyo. Haikuwekwa pale kama Constituency ya Langata. Langata haikuwa eneo bunge mwaka wa 1958. Iliwekwa kama sehemu mbali na mji wa Nairobi yote. Kwa hivyo, Mhe. Mbunge mwenzetu Jalang’o, ni jambo la kuhuzunisha kuona kwamba sehemu yake kubwa pia inatumika kwa wafu ambao moja kwa moja hawamsaidii kupiga kura. Wale walioko pale hawamsaidii. Lakini kama watu wanavyochangia, bado aendelee kupelekewa watu kuzikwa sehemu ile na aone ni vipi atasaidiwa. Maoni yangu ni kwamba, kila eneo bunge la Nairobi hii, kwa sababu Kenya hakuna mahali ambayo sio eneo bunge, wakati County Government ikianza kufikiria suala hili, iweze kutengewa mahali pa kuzika watu. Kwa sababu watu watazikwa na hali ya Nairobi ilivyo, matatizo ya msongamano ya magari, mimi nadhania mtu ambaye atakuwa ametoka sehemu za Kasarani na mahali pa kuzika peke yake ni Langata, kitambo magari yatoke Kasarani yakuje Langata na msongamano wa magari ni huzuni hata kabla ya kufikiria kwamba umefiwa… Kwa hivyo, suluhisho ni kwamba kila pembe la Nairobi iweze kupata maeneo ya kuzika. Na hili pia zitoe nafas,i na serikali ya ugatuzi Nairobi kama ilivyotokea wakati ule, kwamba sasa hao wamepata nafasi ya kupata mchongo pale ndani kwa sababu tunajua ikiwa ni kuzika wafu, mnahitaji ardhi ambayo inafaa. Sielewi kwa nini wakati walinunua shamba la mawe ni kama watu wa Nairobi walikuwa wanataka ujenzi wa mawe ilhali ilikuwa ni sehemu ya kuzika watu. Kwa hivyo, hili pia isiwe imetoa nafasi ya kununua sehemu ambazo moja kwa moja tunajua kwamba hazitafaa na ilhali tunajua kwamba Langata ni mahali ambapo inafaa kufungwa, kuhifadhiwa na kama kuna uwezekano kitaalam, iweze kufanyiwa marekebisho ili watu wa Langata waweze kuishi kwa hadhi inayofaa na waweze kuongezeka. Mhe Spika, ninaunga mkono Hoja hii. Asante kwa kunipa nafasi."
}