GET /api/v0.1/hansard/entries/1278195/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1278195,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278195/?format=api",
    "text_counter": 215,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Hata mimi ninampongeza Mhe. Mwenje kwa kuleta Hoja hii ambayo ni muhimu sana. Haswa, tukizingatia ardhi ni kiungo muhimu sana katika uchumi wa taifa na pia katika mambo ya kilimo. Hata sisi Wakenya lazima tuwe na makaazi katika taifa letu kama Katiba inavyosema katika Sura ya Nne, kwamba lazima Serikali ihakikishe imepatia Wakenya makao. Hatuwezi kupata makao ikiwa hatuna ardhi. Kwa hakika ardhi imekua tatizo nyeti na sugu sana kwa kiasi cha kwamba jamii kwa jamii wameweza kuingia katika vita na mapambano makali. Hata tumeona familia pia zimeweza kupambana na kuwa na mizozo kwa sababu ya suala la ardhi. Serikali iliyoko na pia za nyuma zilizopita, zilijaribu sana kuhakikisha kwamba zimefanya ile tunaita katika Kiingereza Settlement Scheme ama mpango wa makaazi. Hii ni kuhakikisha kwamba Wakenya wamepata ardhi na pia hati miliki. Hivi sasa tukiangalia katika nchi yetu ya Kenya, ukienda sehemu ya bonde la ufa ama mwambao wa Pwani na sehemu nyingine katika taifa letu la Kenya, utapata tuko na maskwota wengi sana. Wengine wako katika ardhi tunazoita kwa Kiingereza, Government Land (GL) ama ardhi za Umma. Kuna wale ni maskwota katika ardhi za watu binafsi ama za watu ambao hawajulikani na hawaonekani. Hii ni kwa sababu tukiangalia historia yetu, hapo nyuma mabeberu walipokuja Kenya, waliweza kunyakua ardhi zetu. Na wengi baada ya kupata uhuru wetu, waliweza kurudi kwa nchi zao na kuacha zile ardhi na kuna watu ambao wameenda na kuishi huko kama maskwota. Mpaka sasa hawajapata hatimiliki. Kuna watu wajanja wanapitiapitia kule wakikusanya pesa na kusema wao ndio wana hatimiliki za zile ardhi ila si kweli. Wanatoza watu pesa nyingi. Imekuwa ni njia ya wahalifu katika taifa la Kenya kupata pesa. Hivyo basi, ni muhimu sana tuangalie takwimu mwafaka kutambua ardhi za Umma zilizo na maskwota, tujue ni ngapi. Je, ni kiasi gani katika kaunti zote 47 za taifa letu? Ardhi ya Umma ambayo Serikali haina matatizo au utata nayo, ipewe Wakenya. Wapewe hatimiliki. Vilevile, Serikali inaweza kutumia fedha ya Land Trust Fund kununulia Wakenya ardhi kwa kuwalipa wanaomiliki zile ardhi lakini hawaishi pale. Ardhi hizo ni maskwota wanaishi mle. Mfano ni ile ardhi ya Waitiki. Mnakumbuka Serikali ya nyuma ilivyofanya. Ninaona Serikali ya sasa iko na mpango na ile ardhi ya Mazrui kule Kilifi. Serikali inanuia kulipa familia ya Mazrui ili maskwota wale wapate ardhi ile. Hili ni jambo ambalo litasaidia Wakenya kupata makao na hatimiliki. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}