GET /api/v0.1/hansard/entries/1278199/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278199,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278199/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Suala hili ni muhimu. Ninajua umeniongezea dakika chache. Kuna pahali muhimu ambapo nilitaka sana kuzungumzia. Tukifanya hivi, kwanza tutapunguza ufisadi wa wale wanaoangalia ardhi ambazo si zao - ardhi za Umma na absentee landlords - ili wazinyakue. Pili, tutapunguza mambo ya professional squatters. Yaani, Wakenya kuwa maskwota kwa muda mrefu. Tutafanya wawe na ardhi. Hivyo basi, kilimo kitaendelea, uchumi utaendelea, na kazi tutazipata. Kwa hivyo, tuzingatie sana kile kipengele cha sheria kinachowezesha mtu kumiliki ardhi anapokaa kwayo zaidi ya miaka 12. Hufanyika hivyo ikiwa mtu hatojitokeza kudai kwamba ardhi ile ni yake. Twawaita, occupants in good faith . Watu hawa wapewe hatimiliki za ardhi hizo kwa msingi huo. Hiyo ndiyo njia pekee itakayotuondolea mizozo, siasa ya mashamba, na kutatua historical land injustices katika sehemu nyingi. Tutaweza kumaliza dhuluma ya kihistoria ya ardhi tukifuata njia kama hizo. Ninakushukuru sana, Mhe. Mwenje. Isiishie kama Hoja tu. Tutengeneze Mswada mwafaka ambao utazingatia na kuwezesha masuala ambayo tumejadili hapa. Sisi kama Wabunge tunafaa kuzika hili tatizo la ardhi katika kaburi la sahau. Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda."
}