GET /api/v0.1/hansard/entries/1278233/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278233,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278233/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza nimpongeze Mhe. Mwenje kwa kuleta Hoja hii kwa wakati unaofaa. Kuhalalisha mashamba kwa maskwota ni jambo la busara na niseme limechelewa kwa sababu wananchi wengi wa Kenya wanaishi katika ardhi ambazo wamezimiliki kwa muda mrefu lakini bado wanaitwa maskwota katika ardhi zao. Utapata kwamba, ardhi nyingi ambazo zimekaliwa na wanaoitwa maskwota ni ardhi za jamii. Ardhi hizi ni za jadi, za mababu na mababu, ambazo kwa sasa inastahili wanaozimiliki waweze kuhalalishiwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}