GET /api/v0.1/hansard/entries/1278234/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278234,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278234/?format=api",
"text_counter": 254,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": "Vile vile, hali hii imechangia unyakuzi wa mashamba. Nikipeana mfano, Magarini kuna mashamba mengi ya chumvi. Mashamba hayo ni ya kukuza chumvi. Lakini baada ya muda, watu wamejiongezea sehemu za ardhi kwa kutumia nguvu zao za kifedha kule katika Wizara ya Ardhi. Wamechukua mashamba ya wenyeji ambayo yamejaa minazi, miembe na mimea mingine. Hali hii imezusha sintofahamu na ugomvi kati ya wenye mashamba ya chumvi na wenyeji. Hoja hii itasaidia mahali pakubwa iwapo tutaipitisha na kuitekeleza. Kupitisha peke yake haitoshi. Tunastahili kuipitisha na kuitekeleza. Kamati ya Utekelezaji ichukue hatua haraka kuhakikisha kwamba huu uhalalishaji wa mashamba kwa maskwota unapata kutimia. Vile vile, hali hii ya uhalalishaji ikaweze kusambaa mpaka kwa mashamba yale ambayo yanamilikiwa na watu ambao hawaishi hapa nchini, kwa kiingereza, absentee landlords . Wengi Magarini, wananchi wamekalia mashamba ya mabwenyenye ambao hawajaishi nchini kwa miaka zaidi ya 100 ilhali bado wanaitwa maskwota. Ninaipongeza Serikali maana imejitolea kununua mashamba hayo ili kuhalalisha maskwota ambao wanakaa humo. Kwenye mashamba hayo tumejenga mashule, misikiti, na makanisa. Ajabu ni kwamba hata makanisa na misikiti ni skwota juu ya mashamba hayo. Iwapo Hoja hii itapita na pia kutekelezwa, basi tutakuwa tumesaidia wananchi wengi. Kuna watu binafsi ambao wamejitolea kutoa mashamba yao kwa Serikali ili iweze kuyanunua mashamba hayo na kuhalalisha maskwota wanaoishi humo. Ningeuliza tu Wizara ya Ardhi iharakishe uhalalalishaji wa mashamba ya jamii katika maeneo ya Adu, Bungale, na Chakama. Hali hii ya kutohalalisha haya mashamba katika eneo la Shakahola, ndiyo imeleta matatizo. Iwapo mashamba yangehalalishiwa wenyewe, ninatumai wengine hawangepata nafasi ya kupenya na kufanya uhalifu ndani ya mashamba hayo. Kwa hayo machache au mengi, ninasema asante kwa kunipatia fursa hii."
}