GET /api/v0.1/hansard/entries/1278360/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1278360,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278360/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika. Nataka kushukuru aliyeleta suala hili. Ningependa kuunga mkono waliopendekeza marekebisho kwa sababu TikTok ni muhimu katika kizazi cha sasa. Kimeleta ufahamu wa watu wengi ambao wameweza kujulikana kimataifa. Kitu ambacho kinasikitisha ni wachache wanaoweka mambo yao ya kibinafsi katika mtandao huu. Mimi siko TikTok, lakini niko katika mitandao mingine yote kama YouTube, Instagram, Twitter na WhatsApp. Ningependa kukufahamisha kuwa mimi ndiye Mbunge wa pekee Kenya hii, ndani ya Bunge hili na Bunge la Seneti, kuchaguliwa kuleta mabadiliko nchini Kenya. Ijumaa hii, nitatuzwa. Nafikiri wale wengine wote wanajua mabadiliko yangu yameenea dunia nzima na nikachaguliwa. Kwa hivyo, mitandao yote ni muhimu. Ujumbe unaokufanya usijulikane zaidi ndio muhimu zaidi. Najivunia kuwa katika mitandaoni, japo sipo TikTok. Nilikuwa naambia Mheshimiwa mmoja hapa kuwa ni wasichana wachache ambao wanataka kujulikana kibinafsi ndiye huweka picha za ngono. Niko tayari kumuunga mkono Mwenyekiti wangu."
}