GET /api/v0.1/hansard/entries/1278539/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1278539,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278539/?format=api",
    "text_counter": 258,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Kiswahili ni lugha tamu sana inayowaunganisha Wakenya na makabila yote. Pia, ninapenda sana kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili ili Wapwani wanielewe vizuri. Nimeuangalia Mswada huu wa leo, ambao ni mzuri sana, tukiangalia maswala ya chakula. Hakuna mwanadamu au mnyama atakayeishi hapa duniani bila ya kula chakula. Lakini cha kusikitisha ni kwamba mashamba yetu yanawekwa madawa ambayo yanaleta madhara katika afya zetu kupitia vyakula tunavyokula. Ninashangaa kwamba ingawaje tuko na Waziri wa Afya, Waziri wa Kilimo na Waziri wa Mazingira, pamoja na KEBS, bado tunatafuta idara ambayo itasawazisha mambo ya chakula cha binadamu na chakula cha mifugo. Hii ni kwa sababu Kenya tumeingia katika mambo ya uvivu. Wahudumu katika idara zilizopewa majukumu haya wamekua wavivu katika utendakazi wao. Ndio maana licha ya kwamba tuna Wizara husika katika nyanja za afya, kilimo na mifugo, Wakenya wanakufa kupitia cancer na food poisoning . Wizara hizi zinafaa kuhakikisha kwamba vyakula vinavyotoka shambani ni salama kwa matumizi ya binadamu. Limekuwa jambo la kawaida kwetu kuleta mijadala na miswada hapa bungeni, tukijaribu kulainisha masuala haya. Wahusika wakuu Serikalini ambao wanapokea mishahara minono wamekaa mahali wanajivinjari. Wanaishi maisha mazuri na kuendesha magari makubwa, huku Wakenya walalahoi wakilishwa vyakula vibovu. Wakenya wanauawa na vyakula vibaya ilhali Waziri wa Afya, Waziri wa Kilimo, na Waziri wa Mazingira wanaendelea kupokea mishahara minono. Nafaka kama vile mahindi, mchele, maharagwe na ngano, ambazo huwekwa kwenye maghala yetu, huwekwa dawa za kuzuia aflatoxins . Hiyo ni wazi kabisa kwa sababu harufu ya dawa hiyo bado huwepo kwenye nafaka hiyo ukienda kuisaga. Wanaokula vyakula hivyo si ndugu zetu sisi tulioko hapa bungeni. Sisi hununua unga chapa ya Amaze ama Hostess, lakini The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}