HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278540,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278540/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "yule mama mpiga kura, na yule anayekatwa ushuru kule mashambani hula chakula kilicho na sumu. Nimeishi katika taifa la Saudi Arabia, na nimeona wakiagiza nyama ya ng’ombe, kuku, na mayai kutoka taifa la South Afrika. Ni kwa nini? Ni kwa sababu wakulima kule South Afrika wanaboresha afya ya chakula katika mashamba yao. Pia, wanaboresha huduma ya mimea katika mashamba yao. Hapa Kenya, utaona ndizi ikitolewa sokoni leo asubuhi, na imeiva kufikia jioni, na iko tayari kabisa kuliwa. Jiulize ni kwa nini nyanya zetu walikuwa wanazifunika ndizi vizuri ili zipate joto na kuiva. Leo hii, ndizi zinatoka sokoni leo asubihi na kufikia jioni, tayari zimeiva. Utazipata ndani ya supermarket, na watoto na familia zetu wanazila. Mhe. Spika wa Muda, hali hii inatamausha sana. Waweza kuchinja ng’ombe leo, na ukichukua hiyo nyama uiweke mahali, inaanza kutoa harufu ifikapo jioni. Lakini ukienda kwenye supermarket zetu, nyama zao siku zote ni nyekundu na fresh kana kwamba zimetoka kichinjioni sasa hivi. Licha ya hayo, Waziri wa Afya amenyamaza. Pia, Waziri wa Kilimo na Mifugo amenyamaza. Mkurugenzi wa KEBS naye huwa amenyamaza. Maanake ni nini? Hii yote ni corruption - corruption ambayo inaregesha Kenya nyuma. Huu ni wakati mwafaka kwetu sisi, kama Wabunge, kupanua mawazo yetu ili Mawaziri wakija hapa kujibu maswali, tuzungumze sote kwa pamoja bila ya kuangalia chama ama kuuliza huyu ni wa wapi. Tukishikana, tutawauliza maswali ya kulijenga taifa hili. Tusijifinye chini na kuwacha Wakenya wakihangaika. Kila siku ninapata case nyingi za cancer ofisini mwangu. Kama mama, ninasikia vibaya kwa sababu Wakenya wanalishwa vyakula na nyama mbovu. Huu Mswada, ambao umeletwa na ndugu yetu, Mhe. Kimani Ichung’wah, ni mzuri sana. Ikiwa wizara na idara zipo, kwa nini tunatafuta ofisi itakayoangalia maswala haya yote wakati kuna watu wamekaa wanalipwa mishahara bila ya kuzingatia usalama wa Wakenya? Ningependa kusema kwamba kama ofisi hii itatungwa na iwahakikishie Wakenya kuwa mambo ya vyakula yataenda shwari, basi tuangalie hizi wizara ili tuone kina nani watafutwa kazi. Tukianzisha ofisi hii, tuwatoe kazini wale ambao hawafanyi kazi zao na hawawajibiki. Mhe. Spika wa Muda, samahani. Nina uchungu kwa sababu mimi ni mama. Ukienda kwenye maternity ward, utapata watoto wanaozaliwa na hali za kutamausha kwa sababu mama zao wamekula vyakula vilivyoingia uchafu, kwanza hapa Nairobi. Samahani, lakini kuna sukuma wiki zimeng’ara kweli ukiziangalia. Lakini ukiangalia utagundua zinapandwa katika maji taka. Chemicals zilizotumiwa katika nyumba za watu zimeingia mpaka mashambani na katika zile mbegu pia. Ile mbegu humea na ule uchafu wote. Zile toxins zote huwa zimeingia ndani, na hii leo, twauziwa hizi mboga sokoni. Watu hawajali afya ya anayekula vyakula hivi itakuwa vipi. Waziri wa Afya na Waziri wa Kilimo na Mifugo wamenyamaza. Leo nitazungumza nikitetea wakulima. Isijekuwa kuna mtu mahali amepiga hesabu vizuri, ashajua mvua inanyesha, na ana mashamba. Mtu huyu anatafuta njia ya ku control vyakula ili apate namna ya kusafirisha vyakula kutoka Kenya akipeleka nje, huku amefungia wakulima wengine. Ikiwa ofisi hii ina nia nzuri, basi kama Mama Mombasa, nitaipigia debe; nitai -support . Sitaiunga mkono ikiwa ina nia ya kudunisha wakulima wetu. Ukiangalia sehemu wakulima hutoka, hali ya sasa inawapatia uvivu wa kuingia shambani. Wamekuwa wakilima vyakula, maghala yamejaa mahindi na mchele, lakini sisi twatoa mahindi na mchele nje. Sukari tunayoleta nchini pia iko na sumu. Je, Bunge hili litakuwa likitunga sheria kila siku, ilhali sisi tulioko Serikalini tunaona vile mambo yanavyotendeka? Kuna usemi unaosema, “Mgala muue, na haki yake umpe.” Tunafaa kuwaheshimu wakulima wa taifa hili. Nimeona wakulima kule Mumias wakilia kwa sababu ya miwa yao kuharibika. Hii ni kwa sababu sukari inatolewa nchi nyingine ilhali wako nayo. Wenye tuko Serikalini tukishakula tunateuka. Unapopumzika nyumbani huku ukinywa chai yako, utasikia kwenye vyombo vya habari kuwa sukari tunayoinywa iko na sumu, na ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}