GET /api/v0.1/hansard/entries/1278541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278541,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278541/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "ile iliyoagizwa kutoka nchi za kigeni. Na kwa sababu tushakunywa, imeingia ndani ya mwili na iliyobaki kwenye mili yetu tu ni sumu. Mhe. Spika wa Muda, Serikali na mawaziri wahusika wanafaa wawajibike. Kama kuna waziri ambaye haelewi kazi yake, aondolewe. Ndio maana tunamwambia Rais aweke watu waliobobea katika sekta fulani. Ikiwa ni sekta ya kilimo, aweke mtu ambaye ni mtaalamu anayejua kuwa shamba fulani au mchanga uko na rotuba kiasi gani. Kama mchanga uko na sumu, na kama maji tunayonyunyizia mimea pia yako na sumu. Hiyo ni kazi ya Waziri wa Mazingira. Ninawaomba Mawaziri wa Mazingira, Kilimo, Mifugo na Mimea wakae pamoja ili waweke vichwa vyao pamoja. Haswa ninawalenga watu wetu wa KEBS wanaoruhusu vitu vyenye sumu kuingia humu nchini. Ninatamaushwa sana, lakini Mjadala huu ni mzuri, na ninaupigia debe. Ninaunga mkono, isipokuwa tunafaa kujua ni kina nani watakaoingia na kuhudumu kwenye ofisi iliyopendekezwa. Ofisi hii isiwe ni ya kunyima Wakenya haki zao. Isiwe ofisi ya kuangalia maslahi ya mkulima mmoja, bali wakulima wote. Nikitia tamati, ninataka kumshukuru sana aliyeuleta Mswada huu. Ninawapongeza wanaosimamia Wizara ya Afya na Mifugo, maana wameshughulika kutengenezwa kwa Mswada huu. Asante sana."
}