GET /api/v0.1/hansard/entries/1278548/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278548,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278548/?format=api",
"text_counter": 267,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Mhe Spika wa Muda, ninakushukuru kwa mwongozo huo. Nitaenda kwa haraka ili wenzangu pia wapate muda na fursa ya kuchangia. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu niko na imani kwamba umetoka kwa Wizara mbili muhimu – Wizara ya Afya, na Wizara ya Kilimo – ambazo zilikaa chini zikakubaliana. Kwa hivyo, niko na imani kuwa hili ni jambo muhimu ambalo litasaidia taifa. Ubora wa chakula ni jambo muhimu sana. Pia, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu utahusisha serikali za ugatuzi katika jitihada za kuboresha chakula kabla ya kukipeleka kwenye masoko yetu. Tuko na imani kuwa wakihusishwa, mambo mengi pia yatakwenda sawa. Ubora wa chakula ni jambo muhimu sana kwa taifa. Chakula salama kinapunguza magonjwa na serikali haitopata uzito wa kuagiza madawa kutoka mataifa ya kigeni. Wananchi watakuwa salama na wenye afya nzuri. Ubora wa chakula ni jambo muhimu sana. Saratani imeenea sana katika taifa letu kwa sababu ya vyakula vinavyotumiwa na watu wetu, ambavyo si salama. Ubora wa chakula unaanzia shambani kwa kuangalia ni mbolea aina gani imetumika, jinsi chakula kilivyovunwa kutoka shambani na kusafirishwa hadi sokoni, ambako wananchi watakinunua na kukitumia. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}