GET /api/v0.1/hansard/entries/1278549/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1278549,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278549/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Wananchi wanategemea mashirika ya kiserikali kuwasaidia kwa sababu hawana uwezo wa kuchunguza vile chakula kimetolewa shambani. Hiyo ni kazi ya mashirika ya kiserikali. Lakini kwa sababu hawashughuliki, na kwa sababu ufisadi umekuwa mwingi, mwananchi anapata chakula kisicho salama kinachosababisha ugonjwa wa saratani na magonjwa mengine. Kwa mfano, kuku wa gredi hupewa dawa fulani, na inabidi wakae siku saba kabla ya kuchinjwa. Lakini kwa sababu hakuna mtu anayechunguza jambo hilo, wale kuku wanachinjwa na kuletwa sokoni ilhali ile sumu bado iko kwenye nyama hiyo, na watu wanakuja wanaitumia."
}