GET /api/v0.1/hansard/entries/1278551/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278551,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278551/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Lakini leo kama walivyosema wazungumzaji wengine, mtu akishamaliza kunywa chai, anaona kwenye runinga kwamba kuna sukari ya sumu ambayo imeingia nchini. Hicho ni kitu cha kustaajabisha. Watu wetu wanapata shida kwa kula sumu baridi. Watu wetu ni wagonjwa. Wewe ingia kwenye matatu, kama hujaingia siku nyingi, uone mtu anatoka kule tumbo languruma utafikiri kwapigwa ngoma ndani. Hii ni kwa sababu chakula ambacho amekula sio salama. Wale wanaotaka kutengeneza ofisi hii wawe ni watu ambao watajitolea. Sisi tunakubali ofisi hii iundwe, lakini wale watakaotekeleza kazi zao ndio hatujui."
}