GET /api/v0.1/hansard/entries/1278810/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1278810,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278810/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Mheshimiwa Spika wa Muda, ningependa kumuelezea Mhe. Kiongozi wa Chama cha Waliowengi kuwa asiwe anajumuisha lawama. Mimi sina shida lakini pengine kunao wengine watakuchukulia vingine na pengine hawana lawama. Kwa hivyo, ukisema wanasiasa, tutafungwa ama nini? Wengine wako upande huo wa kwenu wa Serikali na tunawajua lakini pengine wako sawa. Kwa hivyo, sema wale ambao pengine wanatumia pesa za Umma kuingiza kule na pengine kama unawajua wataje. Usiwalaumu kwa ujumla watu wote ukawaweka katika kikapu kimoja. Wajua unaheshimika sana Kiongozi wa Chama cha Waliowengi na maneno ambayo yanatoka kwenye mdomo wako yanachukuliwa na uzito sana. Usije ukatoka pale mlangoni ukapigwa ngwala. Asante sana Mhe. Spika wa Muda."
}