GET /api/v0.1/hansard/entries/1278894/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278894,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278894/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Keiyo South, UDA",
"speaker_title": "Hon. Gideon Kimaiyo",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Ninamshukuru Mhe. Ruku kwa Hoja ambayo ameleta jioni ya leo. Ninamuunga mkono. Wizara ya Elimu inafaa ituambie vizuri kwa sababu kuna ukosefu wa habari. Mimi kama Mbunge sielewi vile huu ufadhili wa elimu ya juu ulioletwa utatekelezwa. Umesikia jinsi Wabunge wenzangu wamesema. Kama Wabunge hawaelewi vizuri huu ufadhili wa elimu ya juu, yule mtu aliye mashinani atauelewa vipi?"
}