GET /api/v0.1/hansard/entries/1278912/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1278912,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278912/?format=api",
"text_counter": 313,
"type": "speech",
"speaker_name": "Keiyo South, UDA",
"speaker_title": "Hon. Gideon Kimaiyo",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Asante Mhe. Melly. Nimefahamika lakini sikuwa ninakosoa huo mfumo. Nilikuwa ninaangazia zile changamoto ambazo tutazipata hapo mbeleni. Kwa mfano, wiki zijazo wanafunzi watarudi shuleni na watalazimishwa kulipa karo kama hawatafaidika kutokana na huu mfumo wa msaada wa karo. Ninamuunga mkono ndugu yangu Mhe. Ruku kwa kuleta hii Hoja. Ni muhimu sana Wizara ya Elimu itueleze na itufahamishe maanake sisi kama Wabunge, tuna changamoto kuelewa ni nini kitakachofanyika kwa mwananchi wa kawaida. Watupatie habari tupate kuielewa vizuri kwa sababu kuna ukosefu wa habari. Bado tunahitaji taarifa zaidi kuhusu huu mfumo. Njia ambayo imetumika kutambua yule ambaye kwa lugha ya kimombo wanamuita vulnerable inafaa ieleweke."
}