GET /api/v0.1/hansard/entries/1278913/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1278913,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1278913/?format=api",
    "text_counter": 314,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Keiyo South, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Gideon Kimaiyo",
    "speaker": null,
    "content": "Ninamuunga mkono Rais kwa kuleta huu mfumo kwa maana lile jopo ambalo liliteuliwa na Rais ndilo ambalo lilileta huu mfumo mpya. Kule mashinani, mtoto ambaye amesoma kwenye shule ya kibinafsi anashindana na yule mtoto ambaye amesoma kwenye shule ya msingi iliyo chini kabisa. Kwa mfano, mahali ninakotoka kuna shule inayoitwa Kipkanao. Ni shule ya msingi ya tabaka la chini kabisa. Haina madawati, haina madarasa lakini inashindana na shule ambayo ni ya kibinafsi. Mtoto anapita mtihani na alama mia nne kwa sababu amesomea shule ya kibinafsi. Yule ambaye amesoma katika shule ya msingi duni ya Umma anapata alama mia mbili katika mtihani. Yule anaitwa shule ya upili ya Alliance na huyu mwingine anaitwa shule ya Kamang’u. Mzazi wa huyo mwanafunzi anajiweza kifedha kwa sababu alimpeleka shule ya kibinafsi. Wanapomaliza shule ya umma ya sekondari, wanaitwa kwenye chuo kikuu. Wanaenda tena kushindana kwenye chuo kikuu cha Umma. Maoni yangu ni kwamba mzazi ambaye anampeleka mtoto kwenye shule ya kibinafsi pia ampeleke mtoto huyo kwenye shule ya secondary ya kibinafsi na baadaye ampeleke kwenye chuo kikuu cha kibinafsi. Wacha watoto wa Umma walio chini kabisa wapewe fedha za serikali na kusaidiwa kuimarika katika maisha yao ndio wawe sawa na wale wanajiweza kifedha. Tusipofanya hivyo, ukosefu wa usawa katika jamii tunaoita inequality kwa lugha ya kimombo utaendelea kuongezeka. Katika jamii, utaona kwamba wale walio na mali ndio wanaendelea katika maisha yao. Wale ambao hawana mali wanaendelea kwenda chini."
}