GET /api/v0.1/hansard/entries/1279446/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1279446,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1279446/?format=api",
"text_counter": 503,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Spika. Mimi kama Mbunge wa Mombasa aliyepigiwa kura katika muungano wa Azimio ninaunga mkono mjadala huu wa leo ili kuleta uwiano, maelewano, umoja na upendo katika taifa. Kenya imekuwa katika hali tata kwa miaka mingi sana kila wakati baada ya kura. Ningependa kuelezea Wabunge wenzangu kuwa sisi ndio tunawasha moto kule nje. Tumewafanya watu wetu wakapoteza Maisha yao. Ninawaomba haya mazungumzo yanapoendelea, Wabunge waweke amani mashinani, waheshimu vinara wa vyama vyote viwili, na hili nitalisisitiza kwa sababu tumepoteza maisha ya watoto wetu wengi sana."
}