GET /api/v0.1/hansard/entries/1279536/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1279536,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1279536/?format=api",
"text_counter": 593,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Kwanza ninaunga mkono Mswada huu ulioletwa na Mheshimiwa wa Navakholo. Huu ni Mswada mzuri na tunauunga mkono. Kumekuwa na mambo ambayo mpaka sasa hivi yanatuuumiza sana. Mambo mengi ni kwa sababu hakukuwa na mfumo mzuri wa kuangalia sekta hii ya sukari, ndipo sahii tunanunua sukari Ksh350 kwa kilo moja. Haya yote yametokana na mfumo mbaya wa usimamizi, ambao wenzetu wamesema unatokana na kuondolewa kwa Sugar Act na kuja kwa AFFA Act . Katika Mswaada huu, kuna mambo ya utafiti, yaani research, ambalo ni jambo la muhimu sana, na likizingatiwa leo, mambo ya sukari yanaweza kufunguka kwa kiwango kikubwa sana. Leo hii, kuna Kibos Research Institute, ambayo inaangalia mambo haya. Vilevile, katika mambo ya utafiti, sisi pia kule Pwani tunaomba tuyaangalie sana na tujizatiti kama viongozi kuona kwamba tumepigania mambo ya korosho jinsi mambo ya sukari yanavyopiganiwa, kwa sababu yanafanana na haya ambayo yamezungumziwa katika huu Mswada. Mhe. Spika wa Muda, ninaona unacheka kwa sababu kitambo sukari ilikuwa imenoga na mambo yalikuwa mazuri, ndio maana wewe kwa tajriba yako kama mwanasoka, ukatoka kuchezea Kampuni, nafikiri ya Chemilil Sugar. Leo, hakuna mambo kama yale yanayoendelea kule, lakini wakati ule viwanda vilikuwa vimenawiri ndio tuliweza kuzalisha players wazuri kama wewe. Mhe. Omboko, nakumbuka wakati ule tukiwa wadogo, akina Mahmoud Abbas wakiwa AFC Leopards, wewe ulikuwa unachezea Chemilil Sugar. Wewe ulipoupata mpira, mtu alikua anajua kwanza atapigwa kanzu, apate chenga kubwa, na akija atawekwa katikati na akishtuka umefunga bao. Mheshimiwa Spika wa Muda alichukuliwa kwa tajriba ile kwa sababu alikuwa player aliyeinukia wakati ule, na kuwekwa katika timu ya Chemilil Sugar. Tumeangalia kwamba asilimia 45 mpaka 74 ya wakulima wanakosa faida kutokana na mavuno ya mapema. Hilo hutokana na mfumo mbaya ambao ulikuwa pale. Leo, wakulima wa miwa wanalima miwa yao na kuipeleka katika viwanda, lakini badala ya kupata faida, huwa ni hasara. Kule kwetu tunasema wanalima, halafu baadaye inakuwa goji kirba, kirba goji. Yaani wanazungushwa na kuzungushwa badala ya kupata faida. Mhe. Wangwe, Mbunge wa Navakholo, ni rafiki yangu wa siku nyingi kutoka wakati alikuwa akifanya kazi kama transporter kule Mombasa kwa Multiple Hauliers . Wakati ule, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}