GET /api/v0.1/hansard/entries/1279915/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1279915,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1279915/?format=api",
    "text_counter": 360,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Mswada huu. Tangu tupate Uhuru, swala la maji limekuwa nyeti sana. Mpango huu mpya wa kuhusisha Serikali na kampuni binafisi utasaidia pembe zote za nchi kupata maji. Watu binafsi wakihusishwa katika uchimbaji wa mabawa, watasaidia kueneza maji kwote nchini. Mbali na hivyo, sehemu nyingi ni kame na hazina maji. Si kwamba maji hayapatikani; maji ni mengi chini ya ardhi, lakini namna ya kuteka maji haya na kuyaeneza kwa wananchi ni tatizo sugu. Ninatumai kuwa Mswada huu utasuluhisha matatizo hayo, na watu watapata maji kote nchini. Kwa haya machache, asante, na ninauunga mkono Mswada huu"
}