GET /api/v0.1/hansard/entries/1279924/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1279924,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1279924/?format=api",
"text_counter": 369,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii kuchangia hili swala la maji. Ni kweli maji yamekuwa donda sugu kwa sehemu nyingi za Kenya, haswa katika ile Kaunti yangu ya Taita Taveta. Akina mama, watoto, na wazee wanatembea sehemu mbali sana wakienda kutafuta maji. Mara nyingi wakienda kutafuta maji hayo, wanakutana na changamoto nyingi. Tumekuwa na kesi nyingi, hata zingine za akina mama wamepata kukutana na watu wakawatendea vitendo vya unyama hadi kuwabaka kwa sababu ya kutembea msituni kwenda kutafuta maji."
}