GET /api/v0.1/hansard/entries/1282462/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1282462,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282462/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika, tunajua kuna mazungumzo yanayoendelea. Ni lazima yapitishwe katika hili Bunge. Ni muhimu hayo mazungumzo yafaulu ili amani ipatikane nchini. Kulingana na pande zote mbili; Upande wa Walio Wengi na wa Walio Wachache, tunajua wananchi wasio Wabunge walichaguliwa ili wasaidie ile timu ya Bunge. Timu ambayo tulichagua hapa inaongozwa na Wabunge wetu kutoka pande zote mbili. Hawa Wabunge wako na ujuzi na taaluma ya hali ya juu ya kuendesha mazungumzo haya. Vile vile, kuna technical experts ambao wanasaidia hilo kundi. Wao pia wako na taaluma ya juu. Jambo tunalohitaji katika nchi hii ni amani. Bila amani hakuna nchi inayoweza kufaulu katika utendakazi, kuwa na maendeleo, uwiano na kuishi pamoja. Katika Hoja hii, tunasema mazungumzo haya yafanywe kwa njia mwafaka ili yafaulu. Tuko na imani kuwa waliochaguliwa watafaulu katika kujadiliana na kukubaliana na yale yatakayoleta amani humu nchini. Kule kwetu, tunasema majembe mawili yakiwa ndani ya gunia, lazima yagongane. Sio lazima watu wakubaliane na kila kitu katika mazungumzo yoyote. Mazungumzo haya ni ya muhimu sana. Sio lazima watu wakubaliane kwa kila kitu. Lakini, wakikubaliana kwa mambo mengi zaidi, amani ipatikane na Wakenya waishi kwa upendo, watajua ya kwamba sisi sote ni Wakenya na lazima tushikilie Kenya tukiwa pamoja. Hilo litakuwa jambo muhimu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}