GET /api/v0.1/hansard/entries/1282463/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1282463,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282463/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, nia yetu ni kwamba mazungumzo haya yaweze kufaulu. Tuna imani na timu ambazo tumeziweka hapa mbele. Bibilia inatuambia ya kwamba, pale watu wawili au watatu wako pamoja kuzungumza, ni lazima pawe na amani. Kwa hivyo, sisi tuko na imani na mazungumzo haya na vinara wote kutoka upande huu na ule tuliowachagua. Kuna Viongozi wa Walio Wengi wakiongozwa na mhe. Ichung’wa, na Viongozi wa Walio Wachache wakiongozwa na Mhe. Kalonzo Musyoka. Kwa hivyo, mazungumzo haya yataleta matunda na hatimaye Kenya itaendelea mbele na kupata faida kubwa. Bw. Spika, naunga mkono Mswada huu ili uweze kufaulu. Asante sana."
}