GET /api/v0.1/hansard/entries/1282501/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1282501,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282501/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "washachaguwa kwamba wanataka kuwa katika gereza la mazungumzo, kusiwe na utata wowote pale wanapozungumza. Kama alivyosema Seneta wa Meru, iwe ni jambo la mwisho kwa sababu hakuna maana ya uchaguzi ikiwa hakuna mshindi. Vile vile, ni kama tukae sote tuteuliwe tuje hapa Seneti. Tukiendelea hivyo, hata mimi pia niliowashinda kule Kirinyaga watasema kuwe na mazungumzo. Wale walioshindwa ugavana watasema pia kuwe na mazungumzo. Kwa hivyo, iwe ni mara ya mwisho kwamba tunafanya hili. Tukilifanya tumalize, kuwe na amani. Pia wanaongoza wasije kwa misingi na misimamo mikali. Waje na misimamo na kauli zitakazotolewa kwa ajili ya wananchi wa Kenya wala sio kwa ajili ya uongozi. Asante sana, Mstahiki Spika."
}