GET /api/v0.1/hansard/entries/1282538/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1282538,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282538/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Githuku",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13595,
        "legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
        "slug": "kamau-joseph-githuku"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Ninaunganika na wenzangu kuunga mkono Hoja hii ambayo imewasilishwa na Kinara wa Walio Wengi katika Bunge hili la Seneti. Sisi tunaposoma Amosi 3:3 inasema wawili wasipokubaliana, hawawezi kutembea pamoja. Bw. Spika, ninaunga mkono Hoja hii ya kuwa na mazungumzo ya kitaifa ambayo italeta uwiano na kukomeza shida na matatizo yaliyoshuhudiwa katika Jamhuri yetu ya Kenya kwa muda wa siku ambazo kupita tangu tulipokuwa na uchaguzi wa mwaka 2022. Tumeshuhudia vurugu, umwagikaji wa damu na uharibifu wa mali katika Jamhuri yetu ya Kenya. Ninalaani jambo ambalo kama kiongozi kwa sababu limesababisha hasara kubwa katika Jamhuri yetu ya Kenya tukikumba kwamba tulifanya campaign na tukapatia Wakenya ahadi ambazo tutaweza kutimiza. Ukiwa na mambo ya vurugu; umwagikaji wa damu na uharibifu wa mali, unakuta kwamba kiongozi aliyechaguliwa hawezi kuongoza nchi kwa njia inayostahili. Bw. Spika, naunga jambo hili mkono kama ndilo jambo litakaloleta uwiano na amani katika Jamhuri yetu ya Kenya ili Wakenya waweze kufanyiwa kazi. Ninatoka Kaunti ya Lamu ambayo saa hii, imekumbwa na shida na matatizo mengi ya kiusalama. Hili ni jambo ambalo ningependa Serikali iliangalie kwa kina. Kwa nini wananchi wangu wa Kaunti ya Lamu wanauliwa na kuchomewa nyumba kiholela na jamii fulani imekuwa"
}