GET /api/v0.1/hansard/entries/1282548/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1282548,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282548/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa kuchangia Hoja hii ya mjadala wa kitaifa. Najiunga na wenzangu kuwapongeza viongozi wa nchi na wa Azimio, Mheshimiwa ‘Baba’ Raila Amolo Odinga, kwa kuweza kuwa na makubaliano kuhusiana na maswala haya. Wakati kulitangazwa kwamba kutakuwa na mjadala wa kitaifa, nchi ilipumua, biashara zikafunguka na amani ikarudi katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, ni masikitiko kwamba wenzetu hapa wanaweza kuzungumza kwamba ilikuwa haifai kwa viongozi hawa kuwa na mjadala. Tukiangalia hata uhuru uliopatikana katika nchi hii, baadhi ya ndugu zetu walikufa lakini baada ya mazungumzo, kukapatikana mwafaka kule Lancaster na uhuru katika nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika, viongozi wote ambao wametawala nchi hii, wametawala kupitia maswala ya mjadala baina ya viongozi na wananchi. Hakuna kiongozi ambaye alitangaza akaendesha nchi kwa njia ya kiimla. Wale ambao Waingereza wanawaita dictator s ndio hawawezi kukubali kuzungumza baina ya wananchi katika nchi zao. Nchi yetu inaongozwa na demokrasia na Katiba yetu tuliipata kupitia mjadala katika Bomas of Kenya. Kwa hivyo, Wakenya kuzungumza sio jambo geni. Jambo geni ni kwamba tuna Katiba mpya na polisi wanaendelea kuua wananchi kiholela. Hiyo ndiyo hofu ambayo sisi tuko nayo na inaanza kutoka kwa kinara wa nchi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}