GET /api/v0.1/hansard/entries/1282569/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1282569,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282569/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa fursa hii uliyonipa kuchangia Hoja hii ya kuundwa kwa Kamati ya uwiano katika Jamhuri yetu ya Kenya. Ninaunga mkono majina yote yaliyotolewa na upande wa walio wengi na upande wa walio wachache. Kamati hii ni ya mazungumzo ya kuleta uwiano na amani nchini Kenya. Swala la amani ni muhimu sana. Lakini kuwa na amani siyo ukosefu wa vita. Kunaweza kuwa na amani, lakini kuna watu walio na masononeko na manung’uniko mengi. Wakati tulifanya uchaguzi na tukapata Mhe. Rais, kulikuwa na kesi ndogo. Upande wa Azimio ulisema ya kwamba kuna maswala fulani ambayo hawajakubaliana nayo katika uchaguzi. Tulienda mpaka Mahakama ya Upeo. Tuliheshimu matokeo kutoka kwa Mahakama ya Upeo lakini hatukuridhika. Tulisema ya kwamba kuna mambo machache ambayo yanafaa kufanyika baada ya uchaguzi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}