GET /api/v0.1/hansard/entries/1282623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1282623,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282623/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "wakitembea wakiwa wengi wanaweza kuenda mbali, lakini mtu akitembea pekee yake, ataenda haraka lakini atasulubiwa akiwa pekee yake. Ni vizuri kukiwa na haya mazungumzo ili watu waweze kuzungumza. Mimi ni mfugaji. Najua kwamba ng’ombe akishambuliwa na simba, ni vizuri kufuata simba badala ya kupambana na nzi wanaofyonza damu ya yule ng’ombe aliyevamiwa. Sisi tunajua simba ni yupi, aliyeleta shida hizi. Juzi nimemskia akileta vitisho kuwa haya mazungumzo yakivurugwa, basi watu watarudi kuandamana. Sisi tunakashifu haya mambo. Watu wanakuja kwa mazungumzo, tuna Mhe. Kalonzo Musyoka, Mhe. Ichungwa, Kiongozi wa Walio Wengi katika Seneti hii, tunayemuenzi na tunajua atafanya mambo ya busara katika haya mazungumzo. Lakini ikiwa baada ya sisi kusema tumekubaliana watu wawe na mazungumzo, kwa nini vitisho vinaanza kuwa watu wataenda maandamano. Kila mtu anajua shida zilizoko nchini na ni nani anayezileta. Sisi tulikubaliana na watu na wakasonga mbele. Uchaguzi ukafanywa na Mhe. Raisi, akatangazwa. Sasa kuna vijisababu na visingizio kwamba haya mazungumzo yanaelekea kuanguka. Mhe. Mungatana na Mhe. Dullo wamegonga ndipo. Hakuna mahali imesemekana ya kwamba mshindi akishinda anapaswa kukaa chini aongee na walioshindwa."
}