GET /api/v0.1/hansard/entries/1282626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1282626,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282626/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia huu Hoja. Naunga mkono Hoja hii na nawapongeza viongozi kwa kukubaliana kukaa chini kuleta amani ili nchi ipone. Mazungumzo ni muhimu sana lakini yanaweza kuharibiwa na wale ambao wako nje wanaochochea. Tunaomba, hususan sisi viongozi, tuache uchochezi. Tuache Kamati iliyochaguliwa ifanye kazi, ilete ripoti yao ili tuijadili na nchi ipone. Tukianza uchochezi kabla hata mazungumzo kuanza, sioni kama tutafika kokote na mazungumzo haya. Tumeongea sana juu ya vitu kuharibiwa, watu kuuliwa. Ukweli ni kwamba wanaoenda maandamano hawana silaha. Polisi ndio wako na silaha. Wale polisi ambao walisababisha vifo wachukuliwe hatua na waliyouliwa wawe compensated . Wafidiye familia zilizopoteza wapendwa wao. Tunaomba haya mazungumzo yalete natija kwa nchi. Isiwe ni yale mazungumzo ambayo yataturudisha kwa ile Building Bridges Initiative (BBI) iliyofanyika last time. Tunaona mazungumzo haya yakienda kuwa BBI, sioni kama kutakuw na natija yeyote. Tunaomba yawe mazungumzo ambayo yataleta natija, kuponya nchi na kuleta umoja ili nchi iweze kuendelea mbele. Asante, Bw. Spika."
}