GET /api/v0.1/hansard/entries/1282629/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1282629,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1282629/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Yangu ni machache. Itakuwa aibu sana kuwa baada ya miaka tano ya uchaguzi, walio wachache wakishindwa, waende kurusha mawe, kuuwa watu, kufanya mambo mabaya na kila wakati wanakuja kusema tusemezane. Ingawa Biblia inasema watu wawili hawezi kutembea pamoja bila kuelewana, naunga mkono. Hata hivyo, 2027 tutaenda kwa uchaguzi. Nataka mjiandae tukutane pale. Haya mazungumzo yatakuwa ya mara ya mwisho. Pia mnakumbuka katika Biblia, yesu alikuwa anatembea na Judas na hakuridhika mpaka dakika ya mwisho. Mkifikiria mtakuwa kila wakati mnajifanya kama Judas, 2027 tutawatimua mbio na hamtarudia hivo mpaka tuwateme. Jambo la pili, mnasema mambo ya kufungua server . Pia mmeongea kuhusu mambo ya kuua. Mengi mliyoyasema ni nyinyi mmeharibu. Hata mngeulizwa, mvua haingenyesha. Niko na huzuni sana na nyinyi. Mrudi tusemezane, tusikie pamoja, Biblia iwe juu na tutembee safari moja kwa hiki kipindi cha miaka mitano. Asante, Bw. Spika, naunga mkono, lakini sio ile ya Judas na Yesu."
}