GET /api/v0.1/hansard/entries/1283050/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1283050,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283050/?format=api",
    "text_counter": 67,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi nitoe mawazo kuhusu Mswada huu wa mabadiliko ya tabia-nchi. Kule Tana River, kuna kabila linaitwa Wata ambayo kwa miaka mingi walikuwa wanapata maisha kutoka kwa msitu. Sio wao peke yao lakini pia kuna makabila mengi pale kwetu wanaopata riziki yao kutoka misituni. Wiki iliyopita nilikuwa sehemu ya Tana River inayoitwa Chara. Huko watu wamejitolea kusimamia na kuikuza misitu. Hata ile tunaiita Mangrove Forest kwa lugha ya kimombo, wananchi wanajitolea kupitia kwa vikundi vyao kukuza na kuianzisha tena ile misitu inayoharibika kwa sababu ya mabadiliko ya tabi-nchi. Shida iliyoko ni kwamba wananchi hawa hawapati chochote kutokana na kazi wanazofanya. Kinachofanyika mpaka leo ni kwamba kuko na ahadi zinazotokea kutoka kwa Wizara ya Mazingira lakini hakuna kitu ambacho wananchi wanapata. Nasimama kuunga mkono Mswada huu kwa sababu kwa mara ya kwanza, tunaambiwa wananchi wanaohusika na kusimamia mazingari yao, watanufaika. Kwamba Serikali sasa kupitia kwa Mswada huu kutatokea register ya wale wanaosimamia ama wanatoa mchango wao kwa kutunza mazingira kwamba wao watafaidika. Hii pengine ndio hatua kubwa kabisa imefanywa kwa kukuza mazingira yetu. Kwa sababu hadi sasa imekuwa tu ni kama watu wanatoa mwito tukinge mazingira; mwito tusimamie mazingira yetu yawe masafi; tufanye hivi na vile ili tuishi na hali nzuri ya kimazingira. Lakini watu hawaambiwi katika kazi ya mazingira kuna pesa, kwamba ukitunza hiyo miti unaweza kupata pesa. Sasa akili ya mwananchi ikibadilika namna hii, watu wakijua kwamba kusimamia misitu yetu na kupanda miti kuna faida ya kipesa na kwamba kuna register ambayo itawekwa, basi sheria hii itajenga hatua kubwa sana kusimamia mazingira yetu. Bwana Spika, wakati ambao tulikuwa Midrand, Afrika Kusini na wakati huo ambao Rais Ruto alikuja kuongea nasi Afrika Kusini, wajumbe wa Afrika nzima walishangilia sana ilipofika mazungumzo ya mabadiliko ya tabia ya nchi kwa sababu sote tunajua nchi ambazo zimeendelea ndizo zimechafua mazingira, na kwamba nchi ambazo hazijaendelea sana hazina shida ya kuchafuwa mazingira. Kulikuwa na makubaliano katika mji wa Paris kwamba nchi ambazo zimeendelea zitalipa ridhaa kwa wale ambao--- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}