GET /api/v0.1/hansard/entries/1283053/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283053,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283053/?format=api",
"text_counter": 70,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ambayo wanaotoa kule wailipie na sisi tuweke rasilmali zetu na wao walipe. Kwa hivyo ilikuwa hali mpya, akili mpya ambayo inasema kwamba sisi hatutaenda kuomba watu walipe kwa sababu ya uchafuzi wa hali ya hewa. Sisi tutajenga misitu yetu lakini tulipwe kwa sababu ya kujenga hiyo misitu. Watu walishangilia kwa sababu waliona ni akili mbadala ambayo imeletwa. Tunafurahi sana kwamba sasa mashirika, nchi za Kiafrika na nchi za Ulaya, tunakuja hapa Kenya kuzungumzia hili jambo ya kwamba sisi kama Waafrika sasa, hatutataka kuomba. Sisi tuko na rasilmali, wale ambao wanachafua walipie zile efforts tunaweka kusafisha hii anga ambayo wale washaharibu. Ninafurahi sana kuona Mswada huu uko hapa mbele yetu na kwamba wananchi wanaelewe kwamba Senate imekuja kukaa hususan kwa sababu ya kuhakikisha ya kwamba hii sheria ipitishwe watu waanze kufaidi hata kama ni kwa kidogo. Tumeskia hapa kuna mashirika ya kutoka nje Ulaya, wanakuja kwa kaunti zetu na kusema wamefanya mambo ya project za mabadiliko ya tabia ya nchi yetu na wamepata mabilioni ya pesa. Mabilioni yamelipwa lakini wananchi hawajui ni namna gani. Sheria hii ambayo Seneti inapitisha leo itasema ya kwamba, kama kuna project zozote zinafanywa Tana River au kaunti zingine, watu watajua. Kuna register maalum ambayo itawekwa na watu watapata kujua ni project gani, ni pesa ngapi zinaingia kwa"
}