GET /api/v0.1/hansard/entries/1283075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283075/?format=api",
"text_counter": 92,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Kitu cha kwanza ni, naunga mkono Mswada huu wa mabadiliko ya hali ya hewa, au kwa Kiswahili sanifu, mabadiliko ya tabianchi. Kwa mara ya kwanza nimejipata nikiona tabianchi au climate change kwa Kamusi lakini, hali ya hewa ni mojawapo. Bw. Spika, cha muhimu ni kuona ya kwamba tumezingatia swali hili katika nchi yetu. Hii tabia ya nchi inaweza kuangaliwa vizuri ikiwa sisi sote tutajumuika kama Wakenya na kuona tumepanda miti ambayo itaweza kulinda mazingira. Ninatoka sehemu za Kaunti ya Kilifi. Mara nyingi ukienda pande za ufuoni wa bahari, utapata sio kukata miti pekee yake katika ardhi lakini hata ndani ya bahari, mikoko pia tumeikata. Baadaye, tunaona ya kwamba tunaathirika katika ufugaji wa samaki kama kamba ama wadogo wadogo. Ni jambo la muhimu tukizingatia sana hii tabia ya nchi. Vilevile, Kenya hivi sasa iko katika macho ya ulimwengu. Tumeona kwamba wale wanaotawala katika nchi zao, Marais, wengi watakuja hapa wiki ijayo kuongelea swala hili la mabadiliko ya tabia ya nchi. Sisi tukiwemo kama wale walioenda kama nchi tukiwakilishwa katika ule mkutano wa kongamano kubwa lililofanyika kule Paris, tulijiunga na ulimwengu tukakubaliana ya kwamba sisi pia tutakuwa taifa moja ambalo litazingatia mambo ya kuangalia hii tabia ya nchi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}