GET /api/v0.1/hansard/entries/1283079/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283079,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283079/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murang’o",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa hii nafasi. Kwanza, naunga mkono huu Mswada na ningetaka kuchangia kwa njia ifuatayo. Kwa muda mrefu sasa, wakazi na wazawa wengi ambao wanaishi karibu na misitu hawajukuwa wakifaidika na hizo carbon credits kwa sababu kuna wale ambao wanachukulia kama hao ndio wanafaa. Hata kama jamii nyingi zimekuwa zikipatwa na athari tofauti kutokana na wanyama pori na mambo kama hayo, kwa muda mrefu, hawajafaidika na misitu. Kwa hivyo, huu Mswada utaleta natija katika wakazi na wazawa ambao wanakaa karibu na misitu. Wakati miti inahorodheshwa katika hii mambo ya carbon credit, mimea ambayo inalimwa na wakulima kama vile kahawa, minazi na parachichi, inafaa pia iwekwe katika kiwango cha kupewa carbon credits. Ikiwa hivyo, wakulima pia watafaidika kwa njia tofauti hata kama mazao haitakuwa na pesa nyingi sana. Bw. Spika, kuna baadhi ya miti ambayo tunafaa tuiorodheshe itolewe katika kupandwa kwa sababu ina athari kubwa. Kwanza, inaleta madhara makubwa kuliko miti mingine. Miti kama mikaratusi inafaa kuondolewa kwa sababu ililetwa na wazungu kupandwa katika vinamazi kuondoa yale maji mengi ili wapate nafasi ya kulima. Tunafaa tuweke taratibu fulani ya kuondoa miti kama mikaratusi ambayo haifai kupandwa na wakulima kama tutaangalia mabadiliko ya hali ya hewa. Katika hii misitu mahali tunapanda miti, wakulima wapewe nafasi kufanya ufugaji kama wa nyuki. Nyuki ni nzuri katika kuangalia usalama wa chakula kwa sababu wanahusika na pollination. Ni vizuri wakati wale wanakaa karibu na misitu, wakati"
}