GET /api/v0.1/hansard/entries/1283101/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283101,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283101/?format=api",
"text_counter": 118,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada huu wa mabadiliko ya tabia nchi ama hali ya hewa. Bw. Spika, ni vizuri kulinda mazingira. Upanzi wa miti ni wa busara sana katika nchi. Kile ambacho kimekuwa kinavunja moyo ni kwamba mtaala wetu wa masomo hauzingatii zaidi mambo ya mazingira na ukulima. Nakumbuka tukiwa wanafunzi tulikuwa tunazuia mmonyoko wa udongo. Lakini, kila wakati tukipewa motisha tuliambiwa tusome tuwe madaktari, wahandisi na marubani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}