GET /api/v0.1/hansard/entries/1283102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283102,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283102/?format=api",
"text_counter": 119,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Mkulima na wanaojihusisha na mambo ya upanzi wa miti na utunzaji wa mazingira, hawakuchukuliwa kuwa muhimu. Ndiposa wakati huu, nchi ambazo zimeendelea ndizo zinajua ni pesa ngapi watatoa ridhaa kwa kaboni. Hata sisi, sheria tunayoipitisha itasaidia sana. Ukitembea Laikipia, kuna Misitu kama vile, Rumuruti, Lariak na Mukogodo. Lakini, watu walio huko hawafaidiki na misitu waliyonayo. Ukitembea Kaunti ya Kilifi, anakotoka Kiongozi wa Waliowachache, Sen. Madzayo, tuliwaona wananchi wa zile sehemu wakisema hawaoni faida yeyote ya ile mibuyu. Tayari wanaing’oa na kuiuza katika nchi za ughaibuni. Hawaoni faida yeyote. Kwa hivyo, Mswada huu ukipita, tungetaka kujua wale ambao wanakuja kutupatia ridhaa ama fidia kwa misitu. Tusije tukapata watapeli ambao watakuja na hatujui ni pesa ngapi zimelipwa. Tayari wao wameharibu mazingira yao na wakija hapa wao ndio wanatuambia watanunua kaboni kwa pesa ngapi. Tunaishi kwa hali ya uchochole ilhali miti ni yetu na wao wameharibu mazingira yao. Kwa hivyo, ninajua tutakuwa na kongamano kubwa hapa wiki ijayo. Hayo mambo tuyaongee kiwaziwazi. Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. William Ruto kwa kuongea kinagaubaga. Ameyasema peupe kimasomaso na mimi namuunga mkono. Nina imani ya kwamba mambo haya tukiyafuatilia na tukipitisha huu Mswada, watu wetu walio na misitu na shule zetu--- Vijana wametajwa lakini gatuzi zetu zinatajwa katika Mswada huu kwa kupitia tu. Hakuna jambo linalosemwa kwa kindani. Naunga mkono lakini ni vizuri sisi tufuatilie mambo ya fidia kwa kindani. Sio tu kwa makaratasi lakini kwa kusema na kutenda."
}