GET /api/v0.1/hansard/entries/1283103/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283103,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283103/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa fursa hii uliyonipa kuunga mkono Mswada huu unaopelekea kubadilisha sheria ya mabadiliko ya tabia nchi wa 2016 ama Climate Change Act of 2016. Namshukuru Waziri Soipan Tuya. Tulipokuwa na yeye Naivasha kwa mkutano wa Kamati ya Mazingira, aliahidi kueka sera na sheria za kuthibiti uuzaji wa mkopo za kaboni ama carbon credits . Nilifikiri ataleta sheria mpya kabisa lakini katika hekima yake aliamua kubadilisha Mswada wa tabia nchi wa 2016 kipengee cha 23 ili kuweka uthibiti wa mabadiliko ya tabia nchi kwa ile sheria. Hakuna mtu hajaona madhara ya kuharibu mazingira au ya mabadiliko ya tabia nchi. Pale ninatoka, mahali kunaitwa Wundanyi, kuna mahali kulikuwa na mito na imekauka. Kuna mahali watu walikuwa wanachota maji kwa mifereji, lakini sababu vianzo vya maji vimekauka, saa hivi wanatumia magari ama water bowsers. Kwa hivyo, nashukuru sana. Katika Mswada huu ningependa kuangalia Kipengele cha 12 ambacho kinapelekea kueka sera na sheria mufti za kuangalia mkopo wa kaboni ama carbon credits . Kule kwetu Taita Taveta, nafikiri Kiongozi wa Waliowengi Sen. Cheruiyot alitangaza akasema kwamba mkopo wa kaboni mwingi unatoka kule maeneo ya Kasigau, Taita Taveta. Lakini, wale wananchi hawapati faida yeyote. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}