GET /api/v0.1/hansard/entries/1283198/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283198,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283198/?format=api",
"text_counter": 215,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Naunga mkono na naomba Serikali iweze kuwa na upendo wa watu. Kuna mambo inafaa ihitimishwe. Kama ni mambo ya maji kwa kila kaunti; borehole, waterpans na dams, tukipanda hiyo miti kama hakuna hivyo vitu vyote, itakuwa kazi bure. Kama Kaunti ya Embu, tunaunga mkono kwa sababu tunajua miti itatusaidia na mambo yatakuwa mazuri. Kule vijijini, kuna vikundi vya vijana ambao wako na miti mingi sana na wanalia. Serikali nayo inasema kuwa haina mbegu. Ninaomba Serikali isaidie vile vikundi vya vijana wa vijijini waweze kununua hiyo miti, wapande na wawe na mazuri. Tukifanya hiyo kazi yote, tutapata mvua na mambo mengi yatafanyika. Ninaomba Serikali iweke maanani mambo ya magari yanayotoa moshi nyingi sana ndiyo yaweze kufanywa investigations na tukae vizuri. Nikimalizia, ninaunga mkono. Tunaendelea kusemezana mambo ya walio Wengi na walio Wachache. Naomba tusione walio Wachache wakipeana masufuria, itakuwa ni aibu. Katibu Mkuu, ninaomba mawe isiwe kwa mifuko kwa sababu tunajua wageni ni baraka. Tutembee pamoja. Walio Wachache, siku hiyo, mkikuja na mawe, mtakuta mbwa kali pale nje."
}