GET /api/v0.1/hansard/entries/1283697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283697,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283697/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, siwezi kutoa nguo kwa sababu nimeambiwa na Sen. Sifuna nitoe. Hii ni kwa sababu yeye ni mwanaume kama mimi. Shida ambazo tuko nazo katika eneo ya Kirinyaga zinaambatana na ombi ambalo limeletwa katika Bunge hili na Sen. Mwaruma. Ukienda huko Kirinyaga na Embu unapata kwamba walimu ambao wako kwenye mazingira ambayo inafanana, wengine wanapewa pesa za ziada kwa sababu ya kuishi kwenye mazingira magumu na wengine hawapewi. Watoto wa chekechea kutoka Kaunti ya Kirinyaga huvuka mpaka kwenda Kaunti ya Embu ambako kuna lishe shuleni. Ilhali mazingira kwenye Kaunti ya Embu ni sawa na Kaunti ya Kirinyaga. Maswala haya yafaa yazingatiwe kwa njia inayofaa ili kuhakikisha kwamba kuna usawa kati ya walimu ambao wanafunza maeneo yale, ili wasihamie mazingira mazuri, na wanafunzi wanakosa walimu kwa sababu ya pesa za ziada. Bw. Naibu Spika, nitakomea hapo na ikiwa kuna mtu anashida zaidi kuhusu mavazi yangu, anaweza niona kando nimueleze kwa nini nimevaa hivi."
}