GET /api/v0.1/hansard/entries/1283850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1283850,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283850/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Nitarudia jina langu, Murango. Kazi ya mlango ni kufunga ama kufungua. Nimekuja hapa kupinga Taarifa ambayo imeletwa hapa kuhusu, Sen. Orwoba. Hii ni kwa sababu, kuna njia tofauti za kujieleza. Kuna wale ambao wanajieleza vizuri kama Sen. Sifuna. Kuna wale ambao wanakaa katikati kama sehemu nyeti; hawataki kusema upande ambao walipo. Hata hivyo, mimi niko hapa kupinga Taarifa hii kwa sababu tumeona mambo ambayo imefanyika katika hili Bunge hapo awali wewe mwenyewe ukiwa Naibu Spika. Tunakumbuka kuna mambo ilifanyika pale na Seneta wa Migori, kisha ukatoa kauli ambayo tulikuja tukakaa chini na tukaipindua. Hii imefanyika kwa sababu huyu ni mwanamke ama imefanyika kwa nini? Mimi kama baba ya watoto wasichana nimesimama hapa kupinga. Bw. Naibu Spika, maneno inasemekana ilifanywa sio kufanywa. Yale maneno ambayo yalifanywa hatujaiongelelea sana. Lakini yaliyosemwa tumeyaongelea sana. Nakubaliana na adhabu, lakini sio kufukuza mtoto msichana kwa miezi sita kwa sababu ya kauli aliyosema. Sisi wanaume ambao tuko hapa ni mangapi tumesema ambayo hayafai na bado tuko hapa? Nikiangalia Taarifa ambayo imeletwa hapa, imetiwa sahihi na wanaume watano. Waswahili husema katika ‘mahakama ya fisi, mbuzi hapati haki.’ Kuna wakati katika kukosa kufuatilia sheria za Spika, mmoja aliyevunja zaidi ni Seneta tuliye naye hapa, Sen. Cherarkey. Tulikuwa naye hapa na akakaidi amri ya Spika"
}