GET /api/v0.1/hansard/entries/1283861/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283861,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283861/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, Kanuni za Kudumu 122 (a) inasema kwamba kosa moja kubwa sana ambalo unaweza kufanya, nikukosa kutoka nje ukiambiwa na Spika utoke kwa sababu umekosa nidhamu. Ninajua ya kwamba kila kitu tunayosema hapa kuna rekodi maalum. Ninajua hiyo rekodi maalum iko kwa sababu ninachoongea ninajua ni ukweli mtupu. Wakati jambo kama lile lilifanyika, mwenye alikuwa amefanya makosa alikuja akaitwa, kukawa na kikao alafu akarudi baada ya siku moja ama mbili. Tunayeongelea hapa kwa mambo aliyosema, anafukuzwa kwa kipindi cha miezi sita. Bw. Naibu Spika, hata kama kuna makosa imefanywa na mtu yeyote, kipindi cha miezi sita ni nusu mwaka. Majukumu ambayo Sen. Orwoba anafaa kufanya katika Bunge hili yako dhahiri shahiri katika Katiba. Ni vibaya kusema kwamba kwa muda huo wote hafai kukanyaga hapa ama kuhudhuria mambo yoyote ambayo itakuwa inaongelelewa katika Seneti. Kwa hivyo, sikutaja Seneta wa Nandi ili kumkasirisha. Lakini nilikuwa napeana mfano ambao unajulikana. Je, kuna makosa makubwa kushinda mtu ambaye anaambiwa na Spika anyamaze alafu anakuja anatoa"
}