GET /api/v0.1/hansard/entries/1283862/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283862,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283862/?format=api",
"text_counter": 264,
"type": "speech",
"speaker_name": "v",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ibango katika meza na hakupelekwa katika ile Kamati? Tuliona hiyo ikifanyika hapa katika Seneti. Nikimalizia, mghala muue na haki yake mpe. Kila mtu ako na njia yake ya kujieleza. Tunayeongelea kuhusu, Sen. Orwoba, ni msichana mdogo kimiaka. Anafaa kuvumiliwa pamoja na wale wamama wengine ambao wako na umri kama ule. Hiyo ndio kuwapa nafasi ya kukuwa katika hii Seneti. Bw. Naibu Spika, anaweza kuwa alikosea kwa kutojua ama kwa kujua. Hata hiyo, ningeuliza ya kwamba, sisi wenyewe tuko hapa, isipokuwa wale ambao wanadhani sio baba ya wasichana kama mimi. Hata Biblia ilisema ya kwamba asiyekuwa na makosa achukue jiwe la kwanza kumtupia yule mwanamke ambaye anasemekana katika Bibilia. Yesu akasema vile. Na mimi ninauliza hivi; yule ambaye hajakosa katika hili Bunge la Seneti, awe wa kwanza kutupa mawe, kumkashifu na kumfukuza Sen. Orwoba."
}